Jumapili 9 Agosti 2026 - 19:11
Wanazuoni wa Bahrain Wajibu Kauli za Kipuuzi za Mtawala wa Nchi Hiyo Kuhusu Iran

Hawzah/ Mtu anayesema kwamba Umma mmoja una ubora juu ya Umma mwingine katika msingi wa dini hii ni mjinga, au anajifanya mjinga; kwa sababu fadhila zote ni za Mwenyezi Mungu, na kujiona bora miongoni mwa Umma na watu kunategemea tu kiwango cha kushikamana kwao na dini hii, ikhlasi yao na kujitolea kwao katika njia yake.

hKwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, wanazuoni wa Bahrain wametoa taarifa ya kujibu kauli za hivi karibuni zilizotolewa na mtawala wa nchi hiyo kuhusu Iran.

Wanazuoni hao walisema katika taarifa hiyo kuwa: Kilele cha mamlaka nchini Bahrain, kwa kuidharau akili ya wananchi na hadhi ya utume wa mwisho wa Mitume, kimejitokeza na kujaribu kuifanya hidaya ya Mwenyezi Mungu kuwa kama fadhila inayodaiwa na mwanadamu, na kuifanya fadhila ya Mwenyezi Mungu kwa waja Wake wote kuwa ya kipekee kwa Umma mmoja dhidi ya Umma mwingine. Aidha, amepuuza au amejifanya hajui kwamba kuna ukweli thabiti usio na nafasi ya shaka yoyote; kwamba utume wa Muhammad haukuwa wa watu maalumu au kabila maalumu, bali ni rehema ambayo Mwenyezi Mungu aliiteremsha kwa walimwengu wote, Waarabu na wasiokuwa Waarabu, weupe na weusi, kwa usawa.

Taarifa hiyo iliendelea kusema: Mtu anayesema kwamba Umma mmoja ni bora juu ya Umma mwingine katika msingi wa dini hii ni mjinga, au anajifanya mjinga; kwa sababu fadhila zote ni za Mwenyezi Mungu, na kujiona bora miongoni mwa Umma na watu kunategemea tu kiwango cha kushikamana kwao na dini hii, ikhlasi yao na kujitolea kwao katika njia yake. Fadhila hii ni ya Mwenyezi Mungu, si ya mja yeyote miongoni mwa waja Wake, na yeyote anayeshindana na Mwenyezi Mungu kuhusu neema Yake, ni kana kwamba anashindana Naye katika Uungu Wake.

Wanazuoni wa Bahrain walisisitiza kuwa: Kumtii Mtume kwa amri ya Mwenyezi Mungu ni wajibu na ni nguzo kuu ya msingi wa dini hii, na kupitia hilo pekee ndipo ukweli wa kujinasibisha na dini unatofautishwa na uongo wake. Yeyote anayemtii Mtume Mtukufu na Ahlul-Baiti wake, na kuhifadhi uhalisi na usafi wa utume, ndiye anayestahiki zaidi kuwa karibu naye na ndiye aliye karibu zaidi naye. Na hakuna kipimo kingine cha kumkaribia Mwenyezi Mungu Mtukufu na dini tukufu ya Uislamu isipokuwa uchamungu.

Wanazuoni wa Bahrain walimtaka mtawala wa nchi hiyo ajiulize yeye mwenyewe pamoja na watu wake wa karibu: Leo ni nani aliye mstari wa mbele katika Umma na anayetoa mali yake, nafsi yake na watoto wake kwa ajili ya kuutetea Uislamu huu? Ni nani anayepambana na maadui wa Umma na kusimama mbele ya ubeberu wa kimataifa kwa ajili ya kuilinda Quds na maeneo matakatifu? Ni nani aliyeiinua bendera ya Muqawama wakati wengi walipojiondoa kutoka humo?

Wanazuoni hao walisisitiza: Jibu ni wazi kwa kila mwenye utambuzi; ni Jamhuri ya Kiislamu chini ya uongozi wa faqihi mwenye sifa zote zinazohitajika kisheria, pamoja na taasisi zake zote, viongozi wake wa kisiasa na safu zake za wananchi walioungana, ambao wametoa na wanaendelea kutoa kila kitu cha thamani katika njia ya kuutetea Uislamu, Mapinduzi, Serikali na Kiwilaya ya Faqihi wao mcha Mungu na mwenye hekima.

Waliongeza kusema: Mtu anayetaka kuwafanyia Wairani hisani kwa sababu ya Uislamu wao, kana kwamba anadhani kwamba hidaya ya Mwenyezi Mungu ilikuwa zawadi kutoka kwake au kwa watu kama yeye, wala si fadhila tupu ya Mwenyezi Mungu, na anayedai kujivunia Uislamu na kuwa na hamasa kwa ajili yake, anapaswa kujiuliza: Ni Uislamu upi unaokupa wewe na watu kama wewe ruhusa ya kuwafunga, kuwafukuza na kuwatawanya wanazuoni wa Umma, na kuwafuatilia wanafunzi wa elimu za dini na wahubiri wa utume? Unawezaje kupambana na utawala wa warithi wa Mitume, yaani mafaqihi na Mar'aji wa asili wa Uislamu, hadi kuwafuatilia wafuasi wao katika hukumu zao za kidini na kuwaadhibu kwa ukali mkubwa? Je, ni sehemu ya utume wa Kiislamu kwamba ujiruhusu kuwafanyia wengine hisani kwa sababu yake?

Wanazuoni wa Bahrain, mwishoni mwa taarifa yao, waliwataka Wairani na watu wote huru katika Umma huu wamtake mwenye “kauli hizi tupu” asimame katika safu ya kuusaidia Uislamu, badala ya kuudhalilisha, na atumie upanga na uwezo wake dhidi ya maadui wa Umma, badala ya kuwalenga watoto wake waaminifu; na awe mshirika wa Muqawama wa Kiislamu, si msaidizi wa maadui zake. Anawezaje mwenye kauli hizi kujiruhusu kuwa msemaji wa Uislamu na mwakilishi wake, ilhali yeye mwenyewe si hivyo?

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha